Posted by : james Wednesday, November 6, 2019


Sehemu ya 1
Mtunzi HAJJI KASSIM
Mawasiliano na WhatsApp no. 0673063169.

Hii hapa Songa nayo!
Siku ya Jumatatu Asubuh na mapema jogoo akiwika kuashiria kumekucha kuianza Siku mpya ambapo kila mmoja huenda Katika mihangaiko yake kuhakikisha mkono waenda kinywani, wapo waendao shamba, wapo waendao sokon kibiashara, wapo waendao makazini ikiwemo Madocta, Askari, madereva wa magari na boda boda, walimu, na wengine wengi ambao wameajiriwa na serikali na hata waliojiajiri wenyewe kama unavofahamu ugumu wa kipato juu utafutaji wake mgumu mno ila kila mtu anahangaika kuhakikisha anafikisha maisha yake sehemu anapopahitaji
Halikadhalika pia wanafunzi hawapo nyuma kabisa juu ya kuihangaikia kesho yao tena wao ndiyo huw wakwanza kuamka na kukatisha usingizi uliomtamu na huku wapo wanaoacha kitanda bure kwa kukeshea kusoma usiku kucha huku wengine wakiweka miguu yao ndani ya maji kuondoa usingizi, na kuhakikisha wanafikisha ndoto zao na kujenga Taifa Lao Eeeeh mwenyezimungu wape hitaji la moyo wao kwa wenye kujitoa.
"Siku zote Katika maisha Hakuna kitamu bila jasho"
hivyo usikate tamaa wala usisimame Katika ndoto zako kwa sababu umechoka hapana Bali watakiwa kusimama pale unapohakikisha umefanikiwa jambo lako bila KUJALI mangapi wapitia.
Basi leo hii moja kwa moja katika chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) ambapo hukusanya maelfu ya wanafunzi kutoka Katika mikoa mbali mbali nchini Tanzania na hata baadhivyao hutoka nje ya nchi, hapa sasa tunamuona kijana mmoja aitwae JOHNSON akiwa amelala huku akiota ndoto mbali mbali wakati huo huo wenzake huamka na kujiandaa kipindi kinachoanza saa 3:30 asubuhi ila yeye huonekana kuwa sehemu nyingine kabisa kiakili na kifikra kutokana na ndoto anazo ziota.
Rafiki zake wakaribu wa3 JUMMA na JOSEPH wawanaoishi nae room moja yaan hostel moja wenyewe hujiita three "J" kutokana na herufi za mwanzo za majina yao, walishindwa kumuelewa Johnson kabisa maana siyo kawaida yake.
JOSEPH----Aaaah Mwanangu j ndio ulalaji gani huo!?? amka kipindi kinakaribia..... We Johnson!!.... Johnson!!...... Johnson!!. *kimya hakuwa anamjibu Juma alijibia
JUMA ----achana nae bhna muda unakaribia huyo anajielewa anatufanyia kusudi kabisa yaan! Muwache pengine analingia uwezo wake darasani achana nae huyo!
Mara si punde ilisikika sauti ya Johnson,
Johnson---Ooooh please mimi sikujui naomba uniache, niache mimi sikujui, Nilikutongoza tuh kama wanawake wengine! Hapana hapana msiondoke na mimi niacheni! Niacheni!
*hayo maneno yalikuwa yakitoka mdomoni kwa Johnson, rafiki zake wakibaki kumshangaa huku JOSEPH akionekana kucheka mno.
JOSEPH--Hahahaaaa hahahahaaaaa jamaa huyu kweli noma anaota kila kitu tulichokifanya, hahahaaaaa
JUMA---Mmmmh kwani jana mlifanyaje et????
JOSEPH----Jana weekend so tulitoka kidogo alinipeleka sehemu iv nikawa na kunywa kidogo sasa nilimshawishi akitaka asione aibu kutongoza anywe kidogo aaah alipoonja akanywa kabisa basi alilewa vibaya tulipokuw tunarudi njiani tukakutana na mabinti wawili tuligawana mie nimetoka nae yule mmoja lakini kidgo yule demu nikashangaaaa mbona ndiye kama aliyeondoka nae mwenzangu JOHNSON basi nikaona woga nikaachana nae pale pale ila kwakua JOHNSon alikuwa mgeni na pombe alimtongoza na hajagundua Chochote.
JUMA---Mmmmh wadogo zangu siku mtakufa kutongoza tongoza na kupenda penda ovyo ohooo kila Siku huwa nawaambia mnanidharau haya bhna maisha ni yakwenu ila kuweni makini.
JOSEPH--- Mmmmh usitutishe bhna kwanza mm mwenyewe najilaumu nimemuachaje mtoto mzuur namna ile yaani sijui nitampataje ngoja baadae twende kule labda tutawaona tena!
JUMA---Hebu acha utoto tuondoke Bado dakika 10 kipindi kianze darasani.
*haoo kwa pamoja wakaondoka na kumuacha Johnson akiwa amelala!
Juma na Joseph baada ya kutoka darasani wanakutana na Mpenzi wake na Johnson aitwae LILIAN haraka sanaa huulizia juu ya mpenzi wake kulikoni mbona leo hajatokea Darasani!
LILIAN--Joseph rafiki yenu yuko wapi???
JOSEPH ---yuko dom ila usijal yuko pouw tuh
LILIAN--- Basi saw Mwambie baadae atokee kwenye discussion aje na zawadi yangu
JOSEPH--- okay saw usijal shem zimefika hizo byeee! *anapunga mkono kisha hao wa naondoka zao.
Tukiachana na huko leo tuna waona ma bibie wazuur sanaa wakiwa sehemu ya bustani wakula matunda huku wakiwa wanafurah tena huonekana ni Mapacha waliofanana mno kila kitu hata uongeaji wamefanana mno!
Waschana hawa huonekana ni waongeaji mno tena ni waschana ambao ni vigoli hawajui wanaume yaani bado hawajui mapenzi ni nini!!
Huishi na watu hushindwa kuwaelewa sikuzote hufahamika kama ni mtu mmoja kumbe wapo wawili na ili ugundue lazima ukutane nao wote kwa pamoja ila kumjua yupi ndiye YUSRA na yupi YUSFA ni kazi sanaa hata uambiwe wapewa zawadi milioni moja kugundua ni kazi mno.
YUSRA! ---Mmmmh iv kwann wanishaur ni muue yule kijana aliyeitongoza???
YUSFA l---- hahaaa kwasababu yule utakuja kumpenda na sisi miiko yetu kumpenda mtu hairuhusiwi.
YUSRA ----Basi mm naomba yule usimuuwe maan sijui kwann najikuta tuh niko na huruma nae alafu anaonekana ni handsome et eeeeh!
YUSFA--- Wewe unajidanganya tuh kamwe hutaweza maan utakiuka miiko yetu alaf utasababisha Vifo vingi epuka kumpenda maan watakuja kufa hata wasiyo na hatia na ukithubutuh kumpenda mm nitamuua!
YUSRA--hebu achana na hayo tuondoke zetu! *hao Mapacha wawili wakawa wanaondoka zao.
Tukiachana na huko waliko mapacha wakichawi Tunarudi hukua kwa JOHNSON ndio anaamka muda huu sasa na akiangalia saa ya ukutani ni saa 9:50 za jioni looh mungu wangu kweli siku zote hizi ndoto ndoto za mchana siyo nzuri kabisa ukichanganya ja pombe basi bala Tupu!
JOHNSON--- Daah hawajamaa wanaroho mbaya hata kuniamsha sasa hata hivyo na mm ndiyo kulala gani huku jaman dah l!!!
Wakati huo akiwa amechoka kabisa so kabla hajatanabai anashangaa kuona kitambaa cheupe cha peperuka huku kimechorwa ua jekundu na kuandikwa jina lake alafu kikiwa na ujumbe huu! "Johnson hutakiwi kulala na mwanamke yeyote zaidi ya mmoja ambaye ni mimi laa sivyo utaponza maisha ya wasiyo na hatia"
Ghafla kikapotea kipindi akiwa anashangaa shangaa mara rafiki zake wakarudi na kuingia ndani muda huo Huo akaamua kupotezea na ili wasije kugundua kitu!
Basi JOSEPH baada ya kumuona rafiki yake hayupo sawa kiakili na kifikra anaamua kumshauri watoke kidogo akapunguze mawazo na ukiangalia nikweli Kwa kilichomtokea bas anaamua kuondoka na Joseph sehemu za starehe!
Wananunua nyama na vyakula vingine wanakula mara Joseph anamshaur mwenzie wanywe kidogo kuondosha kabisa mawazo basi nae Johnson huamua kunywa kwa siku ya pili tena ndipo anapolewa na kutokujielewa kabisa huku akiropoka ropoka kama unavyojua adabu ya pombe.
mwanafunzi mmoja wakike darasani kwao ambaye mpenzi wake wa zamani na Johnson aitwae Maria anatokea na kumshika mkono kwenda guest kulala nae na kula raha ya mapenzi kumbe hii yote ili kuwa ni mipango ya Joseph kuwakutanisha ili tuh ampotezee mawzo au stress Johnson bas baada ya Hapo Joseph huwaacha na kuondoka zake
Asubuh kunapokucha Johnson wakwanza kumka na akijishangaa kulala na mwanamke ambaye ni mpenzi wake wa zamani na kila anapomuamsha waondoke kimya kila anavyo muamsha waondoke kimy kuja kutaharuki kumbe tayari masikini yamungu weee kumbe yule msichana wa watu MARIA ameshafariki dunia.
....... Itaendelea fuatilia sehemu ya pili......
Mmtunizi Hajji Kassim
Mawasiliano no. 0673063169

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © YUJEM IT SOLUTION - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -