Posted by : james Wednesday, November 6, 2019



Mtunzi Hajji Kassim
Mawasiliano na WhatsApp no. 0673063169

Hiii hapa Songa nayo.
Sehemu ya 2
Bila shaka uko swalama kabisa na kama wasumbuliwa na maradhi basi Allah atakuponya!
Leo Tuanaanzia pale pale Tulipoishia ikiwa JOHNSON yuko Guest na mtoto wakike MARIA
JOHNSON huwa wakwanza kuamka na kuanza kushangaa kivipi sasa niko hapa na nimewezaje kulala na huyu mschana ambayeniliachana nae muda mrefu daah
JOHSON--Daah wee mwanamke wewe mwanamke!!! Amka uondoke kwenu!
Aaaaaah huyu mwanamke vip mbona kmy!!?
*kila anavyomtingisha kumuamsha kimya kila anavyomtingisha kumuamsha kimy! Anaamua kumgusa mapigo ya moyo yameshasimama zamani kabisa looh ndipo anapokuja kutaharuki masikini yamungu wee mrembo wa watu MARIA hayupo tena duniani!
JOHNSON--Anavuta kumbukumbu jana yake ndipo anapokumbuka kuwa alilewa mno! Sasa swali linakuja je yule bibie MARIA kifo kimemkutaje na hakuwa anaumwa wala hana jeraha lolote lile.
JOHNSON--kipindi analia kile kitambaa cheupe kilichowahi kumtokea ambacho kina maandishi haya
"Johnson nimeshakupenda hutakiwi kukutana kimapenzi na mtu yeyote yule zaidi yangu laah sivyo utaponza vifo vya watu wasiyo na hatia"
Baada ya kumaliza kukisoma kile kitambaa kikapotea.
JOHNSON--Sasa anapokumbuka na kushuhudia Yale, anaangua kilio macho yanamtoka pima kichaa kina mpanda sijui afanyeje sasa! Kipindi akifikiria mara mlango unagongwa kuangalia saaa ni saa nne asubuh duh!
Anachanganyikiwa hutoka na nguo ya kulalia hivyo hivyo! Anafungua mlango kwa woga mkubwa na kutaka kupata nafasi ya kukimbia!
Anapofungua mlango kumbe ni mdada wa usafi muda wake aliyo ulipia umeisha anahitaji atoke ili apate nafasi ya kufanya usafi!
Sasa ile anafungua mlango! Yule mdada anataaruk na kupiga mayowe!
"Yallaaaaaah!!!!
JOHSON--kusikia hivyo hurud ndani haraka na kubamiza mlango huku mapigo ya moyo yakienda mbio hofu kubwa ikimtawala huku akinung'unika moyoni mwake!
JOHNSON--Daaah kweli siku yakufa nyani miti yote huteleza, mimi leo kwisha habari yangu huyu mdada ameshajua kama nimeua! Hapa sijui nijiue kabla sijakamatwa! Bas mungu muamshe MARIA afie hata kwao ahaaaaaaaaah aaah mungu wangu!!! Iiiiiiih iiih!
*mara husikia sauti hustuka sanaa!
"Wewe mkaka mie nimekuja kufanya usafi nakuita unatoka na nguo ya kulalia ndio nini sasa!!!!! Muondoke muda wenu umeshaisha nahitaji nifanye usafi wengine waingie! "
Anaposikia hiyo sauti huvuta pumzi
JOHNSON! -- Dah kumbe bado sijajulikana sasa chakufanya hapa ni kukimbia tuh!
Maskini ya mungu Johnson anaamua kukimbia kumuacha MARIA ambaye ameshafariki kwa muda huo!
JOHNSON--mbio mbio njiani anapokutana na massa wa usafi humparamia na kuangusha vifaa vya usafi! Haraka sanaa huwa kuomba msamaha huku akitetemeka
JOHNSON--sorry sorry dadaa aaah!
*huokota vitu kisha huyo huamua kuondoka zake haraka sanaa huku wasiwasi ukimjaa na wakati huo akimuacha na aswali yule mhudumu aliyekuwa akijulikana kwa jina la RODA! Maan uondokaji tuh mtihani kulikoni!?
Basi huamua kuondoka kuendelea kufanya usafi!
JOHNSON-- Anapofika getini hukutana na mlinzi mbavu kweli kweli huanza kuweweseka!
Johnson_shikamoo!
Mlinzi _Hunyamaza kimy!
Johnson hutaka kuondoka mlinzi humuita!
Mlinzi __mbona waweweseka kulikoni!
JOHNSON---Hapana bro! Mimi sijaua wala sina kosa Mimi Johnson tuh!
*kishaa huyo uondoka zake haraka sanaaa
Bsi mlinzi hupuuza kuendelea na mishe zake.
Tunarudi ndani uliko Mwili wa marehemu bibie MARIA! Mfanyakazi huyo ajulikanaeye kwa jina la RODA! Anapofungua mlango humkuta mtu amelala aaah hukumbuka kama kile chumba no. 11 ndicho alikuja kugonga mlango na kutoka kijana mmoja na nguo za kulalia ambaye ni JOHNSON Daah hushangaa na kwajazbq huku akiropoka maneno makali juu ya yule mdada mwenzie tangu alipokuwa mlangoni huku akimsogelea kitandani alipolala MARIA bila kujua kumbe tayar alishakwisha fariki!
RODA! ---weee Malaya usiyejitambua walala lala ovyo kwani hapa uko kwako! Hebu muone alivyokosa Aibu amka huko sisi tufanye kazini zetu! We ndiye kisilaniusiyo na haya hadi saa hizi Mwambie bwana wako akujengee nyumba mfanyie vizuur starehe hapa nyumba ya biashara pesa zenu zimeshaisha haya haya amka!!
*akazidi kushangaa mbona huyo mwanamke hajibii wala haumiii kuamka!
Anaamua kumtikisha hajibiii akaamua kumgusa mapigo ya moyo kumbe ni wajuzi kabisa ameshakwenda mbele za haki Hapo umebaki mwili wake tuh! Ndipo anapogundua kumbe yule ni marehemu! Akikumbuka yule mkaka ambaye ni JOHNSON utokaji wake ni wa hofu na haraka akajua yule ndiye ameua!
RODA! Mbio huku akilia na kujilaumu kumbe alikuw akipigizana ukelele na maiti ilimuuuma sanaa huku akikimbia kuwaita wenzake!
Mlinzi-- nae kusikia ukelele wa RODA haraka sanaaa hukimbilia ndani na kuuliza kulikoni ndipo bibie RODA anapowahadithia kila kitu Mlizni nae hukumbuka uondokaji wayule kijana na alipomuuliza ujibuji wake ulikuwa
"Mimi sijajua wala sina kosa bro! Mimi naitwa JOHNSON! "Hiyo ndiyo kauli ya johnson alipoulizwa na mlinzi
Basi Mlinzi nae hupata majibu na kukimbilia Katika kitanda alichokuwepo yule bibie MARIA ambaye ni marehemu kwa wakati huo!
MLINZI ambaye hufahamika kwa jina la BABUU
Hujilaumu yaan kama kitu cha kujua angelimkamata yule jamaaa ambaye ni JOHNSON! Dah kwa bahati pembeni ya kitanda aliona waleti ya JONSON ambayo ilikuw na hela elfu 30 pamoja na kitambulisho cha mpiga kura! Ilikuw rahisi kuanza kumtafuta Johnson bas haraka sanaa alielekea polisi kutoa taarifa juu ya kilicho tokea Katika guest hiyo iliyoko mkabala na baa pembezon kidogo na Dodoma mjin ambako kilipo chuo kikuu maaruf kwa jina la (UDOM)
Tunarudi kwa Rafiki zake MARIA walioko hostel wanabaki wakizungumza hapa na pale mara si punde simu ya rafiki wa karibu sanaa wa MARIA afahamikae Kwajina la NASRA inaita anapoangalia no. Ni ngeni hutaka kupotezea inaita na kukata, mara inaita tena hadi inakata hapokei huamua kukata na kuweka pembeni, mara inaita tena kwa mara ya tatu et!
Mashoga zake wote kwa pamoja wakaamua kumsema
" Heee shoga si upokee ndio kuringa gani huko!!! Inamaana we mzuri sanaa au pokea simu"
NASRA! ---Aaah hawa ni wasumbufu sanaa wanaume wachuo hapa si unawajua!!! mie huwa sipokei no. Ngeni.
Rafikizake nasra! Pokea kwanza hujui tuh pengine dili la pesa hilo haya ushauri zako!
*Basi kusikia maneno hayo hushawishika na kuamua kupokea simu!
Ndipo anapopokea simu na kuambiwa et MARIA et amefariki na Maiti yake iko hospital ya Dodoma!
Anapokata simu nakuwaambia wenzake wanataharuki
"mbona jana Mara ya mwisho aliondoka guest na Bwana wake JOHNSON! Tena usiku"
kila mtu anabaki kulia na kutaharuki huku wengine wakikimbilia hospitali kuhakikisha!
Chuo kizima taarifa zilizagaa hasa kwa watu wanae mfahamu MARIA iliwauma sanaa maan ni mtu mwenye kuelewana na kila mtu! Na hatawengine wakijiuliza amefariki fariki vip!??? Maaan usiku tu wa kuamka siku hiyo alikuwa mzima wa Afya!
Basi NASRA ambaye ni Rafiki wa MARIA Ambaye hutoka sehemu moja yaani kijijini kwao ni kumoja huamua kupiga simu nyumban kwa kina MARIA huku akilia!
MAMA MARIA!wakati huo akiwa ametoka shamba jembe lake akiambatanisha kufun kwa pamoja na kuni na kubeba kwa Kichw, huku akiwa na chupa ndogo ya maji ya kunywa mkononi!
Basi huamua kusimama na kupokea simu ndipo anaposikia taarifa inayo mshtua sanaa na kutupa mzigo wakuni!
NASRA! ---Mama et MARIA amekufa! *Huku sauti ikitisha kuambatana na kilio kikubwa kinachomshtua Mama MARIA pale pale hutupa kuni taratibu huanguka na kupoteza fahamu!
Tunarudi kwa JOHNSON kutoroka inamuuma maskini ya mungu hubaki na kulia tuh huamua kukimbilia kituo cha polisi kwenda kujisalimisha na kutoa taarifa! Juu ya kilicho tokea!
Anapofika kituoni! Huongea huku akilia na kuingia moja kwa moja hadi ndani kituoni! Anawakuta maaskari polisi nao wanasimama!
JOHNSON-- Jamani mimi sijajua jamani niokoeni mimi ni JOHNSON tuh sijajua! Amekufa mwenyewe tuh!
*looh nani atamuelewa JOHNSON kumbe taarifa zake zilishafika pale anakamatwa na kutiwa ndani kituoni Hapo Hapo bila hata ya kupewa nafasi yakuongea Chochote kitu!
.............usikose kufuatilia itaendeleaaa..............
Mtunzi Hajji Kassim
Mawasiliano na WhatsApp no. 0673063169

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © YUJEM IT SOLUTION - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -