Posted by : james Wednesday, November 6, 2019


Sehemu ya 3
Mtunzi HAJJI KASSIM
Mawasiliano na WhatsApp no. 0673063169

Tulipoishia ndipo tunapoendelea
Hii hapa Songa nayo!!!
*JOHNSON anapoonekana na maaskari anakamatwa nakuwekwa kituoni na anapojaribu kujitetea hamna anaemsikiliza basi kilio chake kinaendelea huku akijaribu kuongea kwa huruma kama kungekuwa na mtu mwenye kuelewa hisia zake aweze kutoka na kuonekana hana hatia! Lakini haikuwa hivyo saw na kutwanga maji kwenye kinu!
Basi tukiachana na huko kituoni alipowekwa JOHNSON Tunarudi kwa Mapacha wawili wakichawi wafahamikao kama YUSRA na YUSFA wakiendelea na mazungumzo yao huku wakionesha kufurahi sanaa juu ya kilichoendelea!
YUSRA--! Mmmh deal done pumbavu na nilikwambia ukimpenda yule utasababisha wasiyo na hatia kufa ona sasa na mm kwenye masuala mazima ya kuua binadamu Niko haraka maan siwapendi sanaa nawachukia maishani kwangu!
YUSFA--heeee hishia Hapo Hapo! Ifike hatamu basi si kila mtu wakumchukia maan binadamu wako tofauti sanaa si kila binadamu basi wakafanana akili na marendo!
YUSRA---- Mmmh ww si useme tuh wajitetea maana umeshampenda JOHNSON na yule ni binadamu wa kawaida haiwezekani kuishi na ww binti wa kichawi!
YUSFA-- anakasirika na kumrushia kisu cha kimiujiza mwenzie, mara hukiona na kukikwepa nae hurudisha mashambulizi wakaanza kushambuliana *huwezi amini visu huchomoka kutoka Katika viganja vyao vya mikono na ni jambo amabalo si lakawaida kwa mimi na ww ambao ni binadamu wa kawaida ila kwa hawa mabinti kwa kuwa ni wakichawi ni rahisi kwao! Hivyo hupambana sanaaaa hatimae mmoja ambaye ni NASRA kuzidiwa nguvu huamua kukimbia nyumban huku akiwa na hasira kali kwa mwenzie ambaye YUSRA na kwa mara ya kwnza hasa Mapacha wa kichawi kupigana, swali linakuja kwann YUSRA hawapendi binadamu wakawaida!??......
Na kwann humuonea wivu mwenzie kisa humpenda JOHNSON......??? tuzid kusonga taratibu utaelewa tuh
Bas Tukiachana na kwa Mapacha hao wawili tunarudi nyumban kwa kina MARIA ambapo ni marehemu kwa sasa huku mwili wake ukiwa hospital ya DODOMA na mama Maria amepoteza fahamu baadae ya kusikia kifo cha mwanae ambaye alikuwa ndiye tumaini pekee Katika familia hiyo ya kimaskini!
Bas baada ya Mama Maria kutupa mzigo wakuni aliyoufunga pamoja na kuni kisha huanguka na kupoteza fahamu
Baba maria wakati huo hajji Chochote Hutupa jembe chini nakumuweka begani kuanza kumkumbiza zahanati ya kijijini kwao huku akilia maskini na kujaribu kuongea na mke wake kipenzi!
Baba maria, ---- Mama maria mke wangu basi naomba usiniache! Ongea Chochote et.... Mama maria acha utani bhna tumeshakaribia,,,,, heheeeeee heeee heeeeeee! Baba maria alisikika mwanaume akikimbia na mkewe mgongoni huku akihema na kukimbia umbali mrefu na hatimae kufika zahanati!
Baba maria --- Jaman nurse naomba unisaidie huyu mtu kapoteza fahamu ghafla tuh nahitaji umsaidie!
Nurse ---- haya saw muweke pale kitandani nakuja kwanza namalizia kula!
Baba Maria --- mmmh ndg yang nisaidie bas mm nitafanyaje. Et!!! Ndgu yangu nisaidie et!
*Mara si punde. Hutokea nurse mwingine na kujibia kwa haraka
Nurse Mwajuma _-----usijal ndg yang mm nipo nitakusaidia!! Pole sanaaa anamuingiza ndani na kuweka madrip huku akiwasiliana na Doctor na pindi anapompigia simu anajibu huku saut za watu wakiwa wanafurah na wakiwa na vifijo nderemo zikifuata
Doctor ---- Hallo!
Nurse --- Halo! Doctor Ben kuna mgonjwa yuko hatarini sanaa na tatizo hili kubwa naomba uje sasahivi!
Doctor ---- saw usijal anzaga mm nakua!
Nurse --- Saw ila naomba uwahi kuja!
*Anapokata simu yanapita masaa mawili doctor hakutokea huku halibya mgonjwa ikizidi kuwa mbaya! Nae Baba Maria akitokwa na machozi huku akizidi kuçhanganyikiwa kwa kinachoendelea
Kipindi Baba Maria wakiwa zahanati wakiendelea kumsubiri Doctor aliyekuwa Katika harusi ya ndugu yake wakati muda huo ukiwa ni muda wakazi,
Sasa tunarud chuoni Nasra na wenzie walijikusanya na kuchangia Gari taarifa ya kifo cha Maria kilitawala huku kila mmoja akijiuliza Katika kumbukumbu mara ya mwisho Maria alikuw na Johnson, sasa iweje afariki na je!!?? Johnson yuko wap?????... Kiukwel hamna aliyetambua ukweli wa hilo na baadhi yao wakijiuliza maswali yaliyokosa majibu huku wengi wao wakiamini huenda JOHNSON amehusika na mauaji hayo kisha akakimbia!
Hatahivyo Rafiki zake wakaribu pia nao wanajiuliza kivip iko hivyo huku JOSEPH akiwa na wasiwasi mkubwa maaan yeye ndiye kiunganishi na mshawishi wa MARIA kwenda kulala na JOHNSON ili kupoteza mawazo kwa rafiki yake sasa kila anavyojiuliza hapati majibu kabisa! Huku maswali mengi akiulizwa na watu juu ya tukio hilo na mahali alipo JOHNSON ila alikosa majibu ya kuwajibu maan nae kwa wakati huo alishakuwa na wakati mgumu!
JUMMA --- Joseph hebu acha kutuigizia twambie mwenzio yuko wap na nilikuwa na waambia hamkutaka kunisikia sasa sikuzote "asiyesikia la mkuu huvunjika guu"
Haya sasa unaona Mtoto wawatu amekufa sijui utafanyaje! Na mara ya mwisho ulikuwa nae ww pamoja na huyo Marehemu MARIA je kulikoni twambie sisi tutakusaidia!
JOSEPH --- mm niliwaunganisha na mtoto alafu wenyewe waliondoka na mm niliondoka ila ukweli sijui kilichotokea!
JUMMA--+Haya si uhutakagi kunisikia mmeponza maisha ya mtu Asiye na hatia!
JOSEPH ----Naomba niache tusisumbuane tumekuja hapa hatujuani so mm nahitaji niondoke hom!
*mara wanavamiana na kutaka kupigana mara watu wanawaamuru wasipigane!
Basi michango chuo ilifanywa na haraka zaidi uongozi wa wanafunzi Amini serikali ya wanafunzi iliinua watu wao na mwalimu wao mlezi safari ikaanza ya kwenda mochwali Katika hospital ya Dodoma fasta fasta wanakamirisha huku zoezi la kutoa mwili wa MARIA na kufunga safari ya kwenda hadi kijijini kwao MARIA maan ni mwendo wa masaaa sita kufika huko kijijini!
Huku wakati huo NASRA akiongoza msafara maaana yeye ndiye mwenye kujua nyumbani kwa kina Maria huku akilia kw uchungu mkubwa sanaaa
Tukiachana na safari ya kuurejesha Mwili wa Maria huku Gari Bus mbili za watu wanafunzi wakiusindikiza mwili wa Maria maana alipendwa na watu wengi na hata wasiyo mjua kwa sura walivutiwa na sifa na watu wanavyoish Na kumuongelea vizuur hivyo kila mtu alitaman kwenda kumzika!
Bas kipindi wako njiani wakieelekea kijijni kwa kina Maria Tunarudi zahanati Alipo Baba Maria wakiendelea kumsubir masaa yalizid kwenda huko na huko ndiyo majira ya saa tano asubuh ndio huyo Doctor na gari lake anaingia na kwenda moja kwa moja kqa mgonjwa kisha humfanyia mlbaadhibya vipimo
Doctor ---- Mzeee huyu mgonjwa wako inahitajika kwenda hospitali ya rufaaaa hivyo katafute usafir!
Baba ----saw Doctor!
*masikini mzeee wa watu hujitoa na kwenda kuitafuta Gari na anapokuja na kufika kunako hiyo zahanati Doctor humuita na kumpa taarifa iliyomshtua Baba Maria
Doctor ---- mzeee inabid ukuwe mvumilivu maji yameshazidi unga mzeeee!
Baba Maria ---aaah yaani sijakuelewa vizuur et nn unahitaji unga au maji Doctor ili mgonjw apone!??....
Doctor!--- humeza mate kisha humwambia,,,, Mkeo ameshafariki tayar so inabid ujikaze!
*Baba maria huwa na wakati mgumu sanaaa basi haina jinsi hulia hatimae hurudisha nyumbani maiti ya mkewe huku akiumia sanaaa kupoteza mkewe kipenzi tena masikini ya mungu wakati huo hajui kilichosababisha mkewe kufa na hajui kama Maria nae ameshakufa mwanae pekee kipenzi leo hii yuko Katika majonzi makubwa ya mkewe kipenzi aliyekufa kwa kukosa msaada wa Doctor kutokana na kuwepo kwenye sherehe ya Harusi muda wakazi aiseee inauma sanaaa doctors kuweni makini na Kazi zenu lakini laa sivyo mtatuuwa kila siku kama Mama maria maaan angewahishwa kupewa msaada wa huduma kwa doctor pengine asingepoteza uhai!
Basi Turubai lilifungwa nyumbani kwa kina MARIA na Halikadhalika watu walijaaa kuandaa juu ya mazishi siku inayofuata huku Baba Maria akilia na kuhitaji wampigie mwanae Maria aliyoko chuoni Dodoma wamfahamishe juu ya kifo cha mama yake mara punde walisikia milio ya Gari zikija,,,, mara Nasra kashuka Analia mara Baba Maria na watu wote walishangazwa na kilio cha Nasra ambaye ni Rafiki wa karibu wa Maria!
Baba maria na wengine walimsogelea Baba Maria alikuwa wakwanza kumuuliza huku wakati huo Nasra alijikuta analia kukosa nguvu na kukumbatiwa na Baba Maria
Baba maria ---- Nasra Bora umerud nyamaza Mwanangu je rafiki yako Maria yuko wap mbona nakuona weye tuh??...
Nasra kugeuka Jeneza likawa linashushwa kutoka kwenye Gari
NASRA--- Baba! Et MARIA ni yule pale akioneshea Jeneza huku akizidisha kulia!
.................... Itaendeleeeeee usikose kufuatilia sehemu inayofuata.........................
Mtunzi Hajji kassim
Mawasiliano na WhatsApp no. 0673063169

Leave a Reply

Subscribe to Posts | Subscribe to Comments

- Copyright © YUJEM IT SOLUTION - Blogger Templates - Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -